Mwongozo kwa wazazi wajawazito na wapya katika muktadha wa COVID-19 bado unaendelea (kwa mfano, bado haijajulikana kama COVID-19 inaweza kuambukizwa kupitia maziwa ya mama), lakini hizi ni nyenzo fupi za muda.
- Ukurasa wa UNICEF, "Ugonjwa wa Virusi vya Korona (COVID-19): Mambo ambayo wazazi wanapaswa kujua": Ukurasa huu, katika mfumo wa "Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara," unafupisha kanuni za msingi kwa wazazi kuhusu maambukizi, kinga na dalili za COVID-19, na unashughulikia mahususi ujauzito na kunyonyesha.
- Rasilimali za CDC: Mwongozo wa Muda juu ya Kunyonyesha kwa Mama Umethibitishwa au Anachunguzwa kwa COVID-19 inatoa muhtasari wa jumla, wakati Maswali na Majibu Yanayoulizwa Sana: Ugonjwa wa Virusi vya Korona 2019 (COVID-19) na Mimba hushughulikia maswali hususa ambayo yanaweza kuwahangaikia wazazi wajawazito.